Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kansiime Ajifungua Mtoto wa KiumeMchekeshaji maarufu toka nchini Uganda, Anne Kansiime amejifungua mtoto wa kiume jana Jumamosi Aprili 24, 2021 na kumpa jina la Selassie.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anne (34) alithibitisha kujifungua kwa ku-share picha inayomuonyesha akiwa kitandani ndani ya hospitali aliyojifungulia mwanae huyo, akionekana kumbembeleza na kusema kuwa anaitwa “Selassie Ataho”.


Pia aliongeza maneno yanayosomeka, “dhambi zake zimesamehewa” Hii ni kama amewakata ngebe mahasimu wake, baada ya kuandamwa kwa muda mrefu na maneno ya kuwa hawezi kushika ujauzito.


Selassie anakuwa mtoto wa kwanza kwa Kansiime na mpenzi wake Abraham Tukahiirwa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments