Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kapombe, Tshabalala Wazua Hofu Simba

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

MABEKI wawili wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomari Kapombe, juzi jioni walishindwa kufanya mazoezi na wenzao kufuatia kukosa utimamu wa kiafya.

 

Nyota hao wawili walionekana kuzidiwa na uchovu kutokana na kucheza michezo mingi mfululizo ndani ya Simba, pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania.Kapombe hakuweza kabisa kufanya mazoezi baada ya kupewa ruhusa ya kwenda kupumzika, huku Tshabalala akipewa mazoezi mepesi kwa muda mfupi na kwenda kupumzika.

 

Kutokana na kukosekana kwao kwenye mazoezi hayo, Gomes alilazimika kuwatumia mabeki Gadiel Michael na David Kameta ‘Duchu’ ambao mara nyingi wamekuwa wakikosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza.Kapombe alipumzishwa baada ya kumfuata Gomes kumpa taarifa ya kusikia maumivu kwenye msuli wake wa kushoto kabla ya kumtaka apumzike kufanya mazoezi.Wakati Kapombe akitakiwa kupumzika, naye Tshabalala alishindwa kuendelea na mazoezi dakika chache mara baada ya kuanza program pale Simba Mo Arena, Bunju, Dar es Salaam.

 

Tshabalala mara baada ya kushindwa kufanya mazoezi, alimfuata Mfaransa huyo na kumwelezea kutojisikia vizuri na kumtaka apumzike.Akizungumzia hilo, Gomes alisema: “Nimewapa mapumziko maalum wachezaji wangu hao baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya taifa.“Nilihofia kupata maumivu zaidi kama wangeendelea na mazoezi wakati tuna mchezo mgumu na muhimu dhidi ya AS Vita.”

STORI: JOEL THOMAS NA WILBERT MOLANDI


Post a Comment

0 Comments