Kenya Yaijibu Uingereza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




SERIKALI ya Kenya imejibu marufuku ya Uingereza kwa kuwawekea raia wa nchi hiyo watakaowasili sharti la kuwa karantini kwa siku 14.

 

 

Raia wa Uingereza watakapokuwa wamejitenga, watahitajika kupimwa ikiwa wamepata maambukizi ya virusi vya corona au la mara mbili siku ya pili na ya nane wakiwa karantini kwa gharama zao wenyewe.

 

 

Pia katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi, ilisema kuwa masharti hayo yanaanza kutekelezwa saa sita usiku wa Aprili 9, 2021. Hata hivyo, ndege za kubeba mizigo kati ya nchi hizo mbili zitaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia masharti mengine yatakayotangazwa.

 

 

Aidha, raia wa Kenya wanaoishi Uingereza au watakaopitia viwanja vya ndege vya Uingereza kuingia Kenya hawataguswa na masharti hayo mapya.

 

 

Hatua ya Kenya imewadia baada ya Uingereza kufanya maamuzi ya kuijumuisha Kenya kwenye orodha ya watakaopigwa marufuku kuingia nchini humo kama njia moja ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

 

 

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya ilisema kwamba hatua iliyochukuliwa na Uingereza inatatiza hasa baada ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

 



 

“Uamuzi uliochukuliwa na Uingereza utaathiri Kenya kwa kiasi kikubwa hasa kibiashara kati ya Kenya na Uingereza, usafiri, utalii na ushirikiano wa kiusalama,” Wizara ilisema.

 

 

Pia wizara ya Kenya ilisistiza kuwa hatua ya uamuzi huo utatatiza shughuli za nchi hizo mbili hasa ikizingatiwa kwamba zimekuwa na ushirikiano wa nyanja mbalimbali kama vile afya, elimu na hata baina ya watu.

 

 

“Zaidi, uamuzi huo wa upande mmoja haukuakisi mantiki na ufahamu wa kisayansi kuhusu ugonjwa huo au kusambaa kwa janga. Badala yake unaonekana kuchochewa na sera ya kubaguzi dhidi ya mataifa mengine na watu wake”.

 

 

Serikali ya Kenya pia ilizungumzia kusikitishwa na kile ilicho kiita ubaguzi wa chanjo ambapo nchi zinazotengeneza chanjo sasa zinabagua nchi zingine na kuamua kijiwekea akiba.

 

 

“Kenya bado imesalia na maoni yake kwamba serikali ya Uingereza ingeiunga mkono kwa kuipatia chanjo. Hii ni baada ya Kenya kuiomba Uingereza kuigawanya chanjo zake ambayo inafahamu kwamba ina idadi kubwa kuliko zile inazotumia kwa sasa”.

 

 

Wizara ya mambo ya nje iliongeza kuwa wimbi la tatu la maambukizi ambalo Kenya inakabiliana nalo sasa hivi na hatua ilizochukua, ni mfano vile Wakenya walivyojitolea kuhakikisha ugonjwa wa corona hausambai ama nchini Kenya au kwingineko duniani.

 

 

Pia Kenya imezungumzia ufahamu kwa kwamba chimbuko la ugonjwa huo sio Afrika, hauna mipaka na wala haujakuwepo kwa muda mrefu kwa mwanadamu kuweza kuelewa mabadiliko ya siku za usoni.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad