Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kila ukiitazama Simba, moyoni unakiri kuwa Yanga bado wana hatua za kupiga..

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Yanga iwekeze kwa Wachezaji 10 wa Kigeni 
.
Pengine tuliwatwisha Yanga mzigo mzito sana msimu huu.. Pengine tulitaka wafanye zaidi ya uwezo wao.. Pengine tuliwaaminisha uongo.. 
.
Lakini ukweli ni kwamba Yanga bado ina safari katika kuunda timu imara ya kushindana na Simba.. Huu ndio ukweli tunapaswa kuwaambia Yanga sasa.. 
.
Kila ukiitazama Simba, moyoni unakiri kuwa Yanga bado wana hatua za kupiga.. Ubora wa Simba uko juu sana.. Kwa kifupi, Simba imekamilika kila idara.. 
.
Kama Yanga inataka kutwaa VPL.. Kama Yanga inataka kufanya vizuri kimataifa, basi lazima warudi kuboresha timu yao.. 
.
Sina shida sana na viwango vya wazawa wa Yanga.. Wachezaji wazawa hawapishani viwango sana.. Ukimsema Nchimbi kwa kushindwa kufunga mwaka mzima, vipi Ajib huko Simba ana magoli mangapi? 
.
Walipofanikiwa Simba ni kupata wachezaji BORA wa kigeni.. Anza kwa Onyango na Wawa.. Lwanga, Bwalya, Chama, Miquissone.. Halafu uje kwa Kagere na Mugalu.. Top players.. 
.
Wachezaji wa daraja la juu sana.. Ni wachezaji wangapi Yanga wanafikia ubora huo? Sidhani kama wanazidi watatu.. Yupo Lamine, Mukoko na Saido.. Pengine labda na yule Yacouba.. .
.
Fiston siyo Mugalu.. Sarpong siyo Kagere.. Carlinhos siyo Miquissone au Chama.. Wachezaji wa kigeni Simba ni bora sana.. Hapo bado kuna Kahata na Chikwende.. 
.
Ninaamini na bado nitaendelea kuamini hilo.. Kama Yanga itapata wachezaji bora wa kigeni, watakuwa na timu bora sana.. Ipo kazi ya kufanya hapa...
.
Kwasasa mechi za Kombe la Shirikisho Afrika zinaendelea.. Mabosi wa Yanga wanatakiwa kutupa jicho huko.. Kuna wachezaji mahiri sana.. Hawa ndio aina ya wachezaji wanaostahili kwenda Yanga.. 
.
Pia Yanga imeona mechi za Ligi ya Mabingwa.. Kuna wachezaji wanafaa sana kule.. Wachezaji mahiri.. Na muda wa kuanza usajili ni sasa.. Yaani Yanga inapaswa kufahamu mahitaji yake ya msimu ujao, na kuona ni wachezaji gani wanafaa.. 
.
Kama Yanga watapata wachezaji bora wa kigeni, msimu ujao sitashangaa kuona wanafanya vizuri.. Sitashangaa.. 

Gift Macha

Post a Comment

0 Comments