Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kim & Kanye Wakubaliana Kutunza Watoto

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURERapa Kanye West amekubali kushirikiana kulea watoto kufuatia ombi la talaka lililowasilishwa naKim Kardashian tarehe 19 Februari, ambalo lilianzisha mchakato wa kumaliza ndoa yao ya karibu miaka saba,

Katika maombi yao wasanii hao wawili nyota, wamekubaliana kumaliza ndoa yao kufuatia tofauti ambazo haziwezi kusuluhishwa, na kwamba hakuna kati yao anayehitaji msaada wa mwenzake .

West na Kardashian wana mabinti wawili -North na Chicago, walio na umri wa miaka saba na mitatu -na wavulana wawili – Saint, miaka mitano, na Psalm, anaelekea kuwa na miezi miwili mwezi ujao. Kwa mujibu wa ombi la Kardashian, walitenganisha mali zao wakati wote wa ndoa yao kutokana na makubaliano yaliofikiwa kabla ya kuoana.

Wanandoa hao ni miongoni mwa mastaa maarufu zaidi duniani na ndoa yao imekuwa mojawapo ya zinazofuatiliwa kwa karibu  hivi karibuni.


Post a Comment

0 Comments