Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kim Kardashian Ajiunga Klabu ya Mabilionea

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREKim Kardashian Ajiunga Klabu ya Mabilionea

 

Nyota wa Marekani wa Kipindi cha TV Kim Kardashian West ameingia katika klabu ya matajiri wakubwa. Utajiri wake umefikia thamani ya dola bilioni moja (£720m) unaotokana na vipodozi, mavazi pamoja na mapato yake ya Kipindi cha TV, mikataba mbalimbali na uwekezaji, Jarida la Forbes limeandika.

 

 

Kwa sasa Kim Kardashian ni miongoni mwa idadi ya watu 2,755 ambao wameainishwa katika orodha ya mabilionea duniani iliyowekwa na jarida la Forbes. Muasisi wa Amazon Jeff Bezos anaongoza kwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola bilioni 177.

 

 

Wamarekani wengine ambao waliongezwa kwa mwaka uliopita ni muasisi wa programu ya mahusiano ya Bumble dating app, Whitney Wolfe Herd ($1.3bn), mtengeneza filamu Tyler Perry ($1bn) na Miriam Adelson ($38.2bn).

 

 

Kim Kardashian West na mume wake ambaye Kanye West alikuwa tayari kwenye orodha kwa kuwa na dola bilioni 1.8 lakini dada yake wa kambo Kylie Jenner aliondolewa katika orodha hiyo mwezi Mei mwaka jana. Jarida hilo lilimshutumu kwa kudanganya thamani ya biashara ya vipodozi.

 

 

Kim Amefanikiwaje Kufikia Hapo?

Jarida la Forbes limejumuisha thamani ya dola milioni 780 iliyoongezeka na kufikia dola bilioni moja inayotokana na biashara yake ya vipodozi na kampuni ya mavazi.

 

 

Kampuni ya vipodozi ya KKW Beauty ilianzishwa mwaka 2017 na kampuni ya nguo ya Skims ilianzishwa miaka miwili iliyopita baada ya kuzindua vazi aliloliita Kimono, ingawa ilishuka kutokana na shutuma za kitamaduni.

 

 

Kardashian West aliuza 20% ya kampuni ya vipodozi ya KKW Beauty mwaka jana kwa dola milioni 200, katika mkataba wa biashara ambao unafika thamani ya $1bn.

 

 

Mradi wake wa sasa wa Skims una nguo za ndani na nguo ndefu na umesaidia katika mafanikio yake. Nyota huyo ametumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zake , sasa akiwa na wafuasi milioni 213 kwenye Instagram; wafuasi milioni 69.7 kwenye Twitter.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments