Kuacha Kuvuta Sigara Kulimfanya Nyerere Kutembea na Kifimbo Kila Aendapo


Wengi waliopata kumuoan mwalimu Nyerere walikuwa wanamuona akiwa Na Fimbo Ndogo mkononi Kwanza ijulikane mwalimu Nyerere hakuwa Na fimbo moja alikuwa Na fimbo nne, ambazo zote wakati wa kutoka nyumbani kwake alikuwa akichagua moja wapo.

WATANZANIA NA DHANA YA MIUJIZA NDANI YA FIMBO YAKE

Watanzania wengi huharakisha majumuisho kuhusu nguvu za Giza au ushirikina, Wengi walipata kusema yafuatayo÷

Nyerere alisahau fimbo yake wakajaribu kuiiba lakini ikawa nzito hakuna aliweza kuinyanyua, mpaka alipokuja yeye mwenyewe.

Wengine wakasema kuwa fimbo ilimwezesha kumtabiria ya mbeleni. Lakin haikuwa kweli hakuna ukweli hata kidogo,

KWANINI ALITAKA KUSHIKA FIMBO?

Jibu ni kwamba mkewe, Maria Nyerere  anasema hapo awali mwalimu Nyerere alikuwa anavuta sana sigara,

Mama Maria anasema "Mume wangu alikuwa na Fimbo 4 nyingine alinunua nyingine alipewa kama Zawadi, lengo la  kutembea na fimbo hiyo ilitokana na nia yake ya kuacha kuvuta sigara, alipotaka kuacha alipewa fimbo kama njia mbadala ya kushika kitu mkononi ili aweze kuacha"- Maria Nyerere.

Kila mtu anajua kuwa mvuta sigara yeyote anakuwa addicted, akiacha anakuwa nervous hasa akiona watu au akiwa anataka kuongea Jambo mbele ya watu.

Hivyo baada ya Nyerere kushauriwa kuacha Kuvuta sigara aliamua kuwa Na kitu cha  kushika Mkononi anapotaka kuongea  na watu au kufanya Jambo, madaktari wanaelewa ilo.

Getrude mongella alisema "Mwalimu alinambia kuwa alikuwa so nervous, kutokana na kuacha kuvuta sigara, hivyo hali hiyo ilimpelekea kuwa mwoga hata mbele ya watu. Kilichomsaidia akishika fimbo anakuwa kawaida, chunguza hotuba zake nyingi mpaka Ashikilie kwa nguvu fimbo yake" alisema mongella,

Hivyo Fahamu kuwa hakukuwa na Uchawi wala miujiza yeyote katika Fimbo ile.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad