Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Lupita Nyong’o Atembelea Serengeti kwa Mara ya Kwanza

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
 

Nyota wa Hollywood kutoka nchini Kenya Lupita Nyong’o ametembelea kwa mara ya kwanza mbuga ya wanyama ya Tanzania ya Serengeti, Aprili 5, 2021. Mwanamitindo huyo muigizaji alipiga picha na kuiweka kwenye mitandao yake ya kijamii na kuandika serengeti.

 

 

Picha hiyo aliyojipiga mwenyewe yaani selfie inaonesha mazingira ya mbuga hiyo na kukiwa na tembo nyuma yake. Miezi michache iliyopita, kulitokea gumzo la kwanini Lupita hakupewa ubalozi wa utalii nchini Kenya na kupewa mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell.

 

 

Lakini waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala alitetea uamuzi wa kumtaja mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell kuwa balozi wa utalii kimataifa kwa nchi hiyo.

 

 

Wakati wa hafla ya umma, Bwana Balala alisema anajua Wakenya wengi wameuliza kwanini muigizaji wa Hollywood Lupita Nyong’o hakuchaguliwa katika nafasi hiyo.

 

 

Waziri akajibu kwamba wamekuwa wakimtafuta Bi. Nyong’o lakini hajapatikana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

 

 

Muigizaji huyo wa Kenya ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar alipendekezwa na Wakenya katika mitandao ya kijamii kuwa mtu sahihi wa kushikilia nafasi ya balozi wa utalii kimataifa kuwakilisha Kenya.

 

 

Bwana Balala alisema Bi. Campbell amechukua nafasi hiyo kwa maslahi ya umma na kwamba serikali inafanyia kazi namna ya kutumia ushawishi wake kutangaza utalii, kulingana na vyombo vya habari vya nchini Kenya.

This is not a Zoom background, I promise! #elphie in the #Serengeti. 🇹🇿 pic.twitter.com/nzMM0qHfyT

— Lupita Nyong’o (@Lupita_Nyongo) April 5, 2021

Post a Comment

0 Comments