Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mabao Yampa Kiburi Msuva

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

MSHAMBULIAJIwa kimataifa wa Wydad Casablanca ya Morocco, Mtanzania, Simon Msuva amefichua kuwa ndoto zake msimu huu ni kuhakikisha anakuwa mfungaji bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msuva mpaka sasa ameshafunga mabao mawili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo huku timu yake ikiongoza Kundi C ikiwa na pointi kumi.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Msuva alisema kuwa malengo yao katika michuano hiyo ni kuchukua ubingwa pamoja na kuwa mfungaji bora kutokana na kuanza vizuri.“Kwanza Wydad ni timu kubwa ambayo itanifanya nionekane zaidi na tunashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa Afrika lakini pia ubingwa wa Morocco.

 

“Lakini nashukuru nimeweza kuanza vizuri na tayari nimeshafunga mabao mawili katika hatua ya makundi na anayeongoza amefunga mabao matatu, sasa matumaini yangu ni kuendelea kupambana ili ikiwezekana niwe mfungaji bora wa michuao hii ambayo itaongeza kitu kwenye wasifu ‘CV’ wangu,” alisema Msuva.

IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments