Mabilionea 18 Afrika orodha mpya ya Forbes, Afrika Mashariki yatoa mmoja pekee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Afrika yajivunia mabilionea 18 utajiri wao wote kwa ujumla ukiwa dola bilioni 74, kulingana orodha mpya iliyotolewa na jarida mambo ya kibiashara na utajiri la Forbes.

HISTORIA YA MO DEWJI (MOHAMMED GULAM DEWJI) - www.janjastory.com

Kwa mujibu wa orodho iliyotolewa jana Jumanne, Aliko Dangote wa Nigeria anaendelea kuongoza kwa utajiri kwa mwaka wa 10 mfululizo huku utajiri wake ukiwa dola bilioni 11.6. Hata hivyo, Dangote ni wa 190 katika orodha ya matajiri wa dunia nzima.

Barani Afrika, Dangote alifuatwa na Nassef Sawiris wa Misri utajiri wake ukiwa ni dola bilioni 8.5, Nicky Oppenheimer wa Afrika Kusini akiwa na utajiri wa dola bilioni 8, Johann Rupert wa Afrika Kusini akiwa na dola bilioni 7.2 huku Mike Adenuga wa Nigeria thamani yake ikiwa ni dola bilioni 6.3.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Mtanzania Mohammed Dewji pekee ndiye aliyeingia katika orodha hiyo.

Ingawa idadi ya matajiri hao katika jarida la Forbes iliongezeka kote duniani huku ikiweka rekodi kwa kuongeza watu wapya 493, idadi ya mabilionea wa Afrika ilipungua kidogo ikilinganishwa na mwaka 2020 ilipokuwa 20.

Mabilionea 18 wa Afrika wanatoka mataifa mbalimbali kama vile Afrika Kusini na Misri zikiwa na matajiri watano kila mmoja, Nigeria ikiwa na matajiri watatu, Morocco matajiri wawili, Zimbambwe, Tanzania na Algeria wakiwa na tajiri mmoja kila mmoja.

Orodha kamili ya mabilionea wa Afrika kwa mujibu wa Forbes:Je Dangote kuinunua Arsenal?

Dangote ameendelea kuwa mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka wa 10 mfululizo
1. Aliko Dangote – Nigeria – ana thamani ya $11.6b

2. Nassef Sawiris – Misri – ana thamani ya $8.5b

3. Nicky Oppenheimer – Afrika Kusini – thamani ya $8b

4. Johann Rupert – Afrika Kusini – ana thamani ya $7.2b

5. Mike Adenuga – Nigeria – ana thamani ya $6.3b

6. Abdulsamad Rabiu – Nigeria – ana thamani ya $ 5.5b

7. Issad Rebrad – Algeria – ana thamani ya $4.8b

8. Naguib Sawiris – Misri – ana thamani ya $3.2b

9. Patrice Motsepe – Afrika Kusini – ana thamani ya $ 3b

10. Koos Bekker – Afrika Kusini – ana thamani ya $2.8b

11. Mohamed Mansour – Misri – $2.5b

12. Aziz Akhannouch – Morocco – $2.0b

13. Mohammed Dewji – Tanzania – $1.6b

14. Youssef Mansour – Misri – $1.5b

15. Othman Benjeloun – Morocco – $1.3b

16. Michiel Le Roux – Afrika Kusini – $1.2b

17. Strive Masiyiwa – Zimbabwe – $1.2b

18. Yaseen Mansour – Misri – $1.1b


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad