Majizzo afunguka kuhusu kufunga ndoa kimya kimya




 Kwa mara ya kwanza, Mkurugenzi wa E-FM na TV-E Majizzo amefunguka juu ya ndoa yake na Muigizaji wa Filamu nchini Elizabeth Michaell maarufu kama Lulu, kwanini ilikuwa kwa mshangao 'surprise' na kwanini ilikuwa ya watu wachache.
Akizungumza leo kupitia kipindi kipya cha Joto Kali La Asubuhi na Mtangazaji Gerald Hando, Majizzo amesema, 

"Kwanza nilitaka kuwaonesha vijana kwamba unaweza kufunga ndoa hata kama una kitu kidogo. Mimi ningeweza kuwa na watu zaidi ya elfu 3 lakini nilitaka nisiwatishe, harusi haikuwa ya gharama (ukiachilia mavazi) alisema Majey.

Aliendelea, "Lakini pia nilitaka kufanya jambo la kiroho tu. Wazazi walitupa 'support' kubwa. Mimi nina marafiki wengi ningetaka kuchangisha wangejaa, Elizabeth Michaell naye ana marafiki wengi Bongo Movie yote wangejaa." - Majizzo.

Itakumbukwa, Februari 16, 2021 majira ya saa 10 Alasiri zilisambaa taarifa za wawili hao kufunga ndoa baada ya picha wakiwa kanisani kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad