Makamu wa Rais Dk. Mpango atoa msisitizo kwa TRA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka Watumishi wote wa Umma na Watanzania kufanya kazi kwa Bidii, Uadilifu na weledi pamoja na  kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

 

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo April 04,2021 katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.


Aidha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria za Nchi na kuwaacha Wafanya Biashara wafanye Biashara zao kwa  Haki na kutowanyanyasa kwenye Biashara zao ili kuleta kodi kwa ajili ya kuweza kuwahudumia Watanzania.


Katika Ibada hiyo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pia amewasilisha salam za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaomba Waumini hao na Watanzania kwa ujumla waendelee kumuombea Rais Samia na kuiombea Nchi ili iweze kuneemeka zaidi  ya hapa ambapo Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametufikisha.


katika salamu hizo Mhe. Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka na kuendelea kufanya kazi ili kuweza kuijenga Nchi yetu ya Tanzania.

 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad