Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mastaa wa Kike Waliowahi Kudumu Penzini na Mondi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


WANASEMA raha ya mapenzi ni udumu na mwenzi wako kwa muda mrefu lakini pia akuweke hadharani ili ndugu jamaa na marafiki wakujue, sio unafichwa fichwa kama utumbo wa ndani.


Leo nimeona nikuletee makala haya inayowahusu mastaa wa kike ndani na nje ya nchi ambao wamewahi kuonja penzi la kijana anayefanya poa kunako gemu la Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa muda mrefu na kisha kuachana.


Wema Sepetu Alijizolea umaarufu zaidi baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2006, akazidi kupata umaarufu mkubwa baada ya kujiingiza katika soko la filamu akiwa na marehemu Steven Kanumba.


Unaweza kusema ni kipenzi cha watu wengi Tanzania kutokana na sauti yake nyororo, urembo na roho nzuri aliyojaaliwa ya kumjali kila mtu anayekutana naye, mrembo huyu miaka ya nyuma kidogo alishika sana vichwa vya habari baada ya kuangukia katika penzi la Diamond.


Walidumu kwa miaka kadhaa na ni ukweli usiopingika kwamba hii ndio ilikuwa kapo pendwa Bongo kuwahi kutokea, lakini kwa bahati mbaya kila mmoja hakuwa ridhiki kwa mwenzie hivyo wakaachana mazima.


Penniel Mungilwa ‘Penny’Ni mtangazaji maarufu Bongo amewahi kufanya kazi katika televisheni ya Dtv na Efm ambapo huko ndio umaarufu wake ulipoanzia, akaja kung’aa zaidi na kuzungumziwa kila kona baada ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Diamond, hata hivyo na wao baada ya kudumu kwa miaka kadhaa wakaja kuachana na kila mmoja kushika hamsini zake.


Zarinah Hassan ‘Zari the boss lady’ Huyu ni mjasiriamali toka nchini Uganda mwenyewe hupenda kujiita boss lady kutokana na maisha ya kifahari anayoishi, awali hakuna aliyekuwa akimfahamu lakini baadaye baada ya kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na Diamond ndipo watu walipoanza kumfuatilia kwa ukaribu.


Mwanamama huyu ndiye aliyekuwa staa wa kwanza kumzalia msanii huyo mtoto wa kwanza wa kike aitwaye Latifah Nasibu ‘Tiffah’ kisha baadae kumuongezea mtoto wa pili wa kiume aitwaye Nillan Nasibu ‘Prince Nillan’.


 


Hata hivyo, penzi lao halikudumu kwa kile kilichodaiwa ni usaliti ambapo waliachana na kila mmoja kuendelea na maisha yake mengine ambapo kwa sasa wamebaki kuwa walezi tu.


 


Hamisa MobetoNi mwanamitindo maarufu Bongo, naye alianza kuingia kwenye midomo ya watu wengi baada ya kumzalia Mondi mtoto wa kiume aitwaye Dylan na kisha kusema hadharani kuwa alifahamiana na staa huyo miaka kumi iliyopita kipindi yupo na Wema hivyo anamjua nje ndani.


 


Tanasha Donna Baada ya kupita sehemu zote hizo staa huyo wa Bongo Fleva alijikuta akizama tena kwenye penzi zito la mwanadada kutoka nchini Kenya Tanasha ambaye naye walidumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi kadhaa hivi na baadae kujaaliwa mtoto wa kiume anayefahamika kwa jina la Naseeb Juniour ambaye wamefanana ile mbaya.


 


Lakini kama wasemavyo wahenga kuwa kisicho riziki hakiliki, ndicho kilichomtokea mrembo huyo ambapo baada ya muda walimwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake na sasa wamebaki kumlea tu kijana wao huyo.


 


Nafasi iko wazi?Baada ya kijana Mondi kubanjuka na warembo wote hao sasa hivi anasema kuwa yupo singo na pia hatakuwa tayari kutangaza mahusiano yake yoyote yale mpaka pale atakapo kuja kumpata mwanamke wakumuoa, swali ni Je? Kweli yupo singo?


Yaani nafasi ipo wazi? Maana mmmh! Kazi kwenu wadada.


MAKALA: MEMORISE RICHARD | UWAZI

Post a Comment

0 Comments