Meneja wa Simba: Tuliyojiwekea yametimia!
Meneja wa kikosi cha wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika, klabu ya Simba, Meneja Patrick Rweyemamu amesema wanashukuru Mungu mipango waliyojiwekea yote imetimia kwenye upande wa michuano hiyo mikubwa afrika.


Rweyemamu ameiambia EATV mchana wa leo Aprili 15, 2021 kuwa, Uwezekaji uliofanywa kwenye klabu ya Simba mpaka hivi sasa ndiyo siri ya mafanikio ya klabu hiyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Akizungumzia suala la Simba kufuzu robo fainali yamichuano hiyo, Rweyemamu amesema,“Huu ni takribanbi mwaka wa tatu mfululizo tunashiriki kwenye haya mashindano, na unajifunza kwenye kila hatua unayoendana nayo. Tulianza tukafika robo fainali, tukaja tukatolewa kwenye mashindano kwenye hatua ya awali, tumekuja safari hii kufika robo fainali tena na Mungu akijalia Inshallah tutafika nusu fainali”.“Kwahiyo huu ni mchakato ambao lazima tuishukutu taaisisi nzima ya Simba Sporst Club, kuanzia mwekezaji, tushukuru kuanzia benchi la ufundi, kuanzia bodi nzima, kuanzia wachezaji na wapenzi na wadau kwa ujumla wao. Ni kitu ambacho tumekidhamiria, ni suala la uwekezaji hakuna amabcho kilichotoka hewani la msingi ni kushukuru mipango tuliyojiwekea yote imetekelezeka.”Simba imefuzu hatua ya robo fainali mara mbili ndani ya misimu mitatu na sasa inasubiri droo ya hatua hiyo inayotaraji kuchezeshwa tarehe 30 Aprili 2021 nchini Misri ili kujua atapangwa na klabu ipi kati ya CR Buelizdad ya Algeria, Horoya ya Guinea na MC Alger ya Algeria.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad