Mguu Uliojaa Pingili za Mifupa ulifanya Msimamo wa Ligi kuu Kubadilika

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Mguu uliojaa pingili za mifupa ulifanya msimamo wa ligi kuu Tanzania baada kubadilika ,ukaifanya mechi ya Yanga na Azama kuwa tamu kuliko ule ulimi wa Dr Kumbuka,ukaufanya moyo Haji Manara kuota pembe ukamfanya Jimmy Kidoki kutamani kubadilika mithili ya kivuli cha Dulla Makabila na zaidi ukaifanya jioni ya futari ya mashabiki wa simba kuwa muhimu kuliko simulizi ya kimbunga jobo.

Mguuu huu ulikuwa wa kijana Mohamed Hussein ambaye aliamua kuuzamisha uwanja Gwambina complex mbele ya mboni za macho za wasukuma waliokuwa wameshiba sato,na zaidi aliamua kuikausha sauti tamu ya Baraka Mpenja baada ya kufunga goli ambalo liliifanya ile hadithi ya Injia Hersi ya kubebwa mithili ya Kinjeketile Ngwale kufika katika ukomo wake.

Goli hili la Mohamed Hussein pale juu ya ardhi ya misungwi lilibeba mzimu wa kimbunga jobo,liliashiria kwasasa kwenye klabu ya Simba miguu yake ina thamani zaidi kuliko kipaji cha soka kilicholala usingizi mtamu kwenye hisia za Clotus Chota Chama,kuliko hata ile sauti ya Haji Manara ambayo mara nyingi uwafanya mashabiki wa Yanga kutamani kugeuka mawe.

Mguu wa Mohamed Hussein baada ya jana kumtoa Nugaz machozi utaishi milele kwenye historia ya Simba,Daima utamaliza bundle la Mo Dewji,utamfanya pia Barbara Gonzalez kuzungumzwa sana mithili ya Kimbunga Jobo, na zaidi utamfanya kuwa moja ya Ceo ambaye anapaswa kupewa tuzo ya Malkia wa Nguvu kwasababu walau amefanikiwa kuifanya Simba kuiweka Kariakoo Mfukoni.

Goli lake litakuwa mzigo mzito kwenye mtandao wa instagram kuliko hadithi ya kajala na Paula,litatufanya tusahau kuwa Rayvann aligusa hisia za Kondeboy, na labda ule wimbo wa attitude itabidi tuutazame baada ya chungu,chachu na tamu za goli la Mohamed Hussein kumaliza uhai wake kwenye dunia ya soka,na labda siku Kikombe cha Vpl kikiwa kimesimama mbele ya ofisi za Mo dewji.

@omarrkombo

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad