Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mkaongeze walipa kodi- Rais Samia

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Fedha na Mipango kwenda kuongeza idadi ya walipa kodi na kutokutumia nguvu nyingi katika ukusanyaji wa mapato.


Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Katibu Mkuu Kiongozi leo, Jijini Dodoma amewataka kwenda kutanua wigo wa walipa kodi.


''Naomba mkaongeze walipa kodi, hii 'trend' mnayoenda nayo si nzuri, mnatumia nguvu sana kuliko akili katika kukusanya mapato, mnaowachukulia vifaa vyao na kufunga akaunti wakitoka hapo wanaenda kufunga biashara wanahamia nchi ya pili,'' alisema Rais Samia.


Aidha, amewapongeza mawaziri kwa kuendelea kuwepo katika kusaidia majukumu mbalimbali na kuwataka wakafanye kazi kwa pamoja ikiwa wapo kwenye bunge la bajeti kwani bila bajeti ya serikali hakutokuwa na fedha.


''Niwapongeze mawaziri wote kwa kuendelea kuwepo kwenye kusukuma jahazi letu. Niwaambiwe jahazi hili upepo uzidi au uwe mdogo ni lazima liende,'' alisema Rais Samia.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments