Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mobeto Rick Ross Wazua Jambo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Hamisa Mobeto juzi amefanya mahojiano ya moja kwa moja (live) katika kipindi cha Self Made kinachorushwa na mkurugenzi wa kinywaji cha Belaire, Brett Berish, huko nchini Marekani.

 

Wakati mahojiano hayo yakiendelea ghafla msanii mkubwa toka nchini Marekani, William Leonard Roberts ‘Rick Ross’ akatuma ujumbe mfupi uliosomeka hivi ‘We love Misa too’ akimaanisha wanampenda Hamisa pia, jambo lililoibua gumzo kwa baadhi ya mashabiki wa mrembo huyo, huku wengi wao wakihoji ukaribu wa mastaa hao ulianzia wapi.

 

“Ina maana Mobeto anajuana na Rick Ross kitambo? Ni kama wanajuana maana sio kwa komenti hiyo, haya kama wanafahamiana basi ni jambo jema tutegemee kuona kazi nyingi zaidi kutoka kwao,” shabiki mmoja aliandika mtandaoni.Self Made ni kipindi ambacho kinawaibua watu ambao wamefanikiwa kwa kutumia nguvu zao wenyewe, ili kutoa somo kwa watu wengine ambao wanataka kufanikiwa kama wao, Brett ambaye ndio bosi wa kipindi hicho tayari mpaka sasa ameshafanya mahojiano na watu maarufu kama vile Yemi Alade, Tekno, Lil Wayne na wengineo.


Post a Comment

0 Comments