Mpango wa kumaliza malaria Zanzibar umeanza kazi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






Na Thabit Madai, Zanzibar.

MPANGO  wa kumaliza Malaria Zanzibar wakishirikiana na Kamati za Shehia za kuimarisha usafi na kuondosha mazalia ya mbu wamefanya usafi katika shehia za Kikwajuni bondeni ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Afrika.



Maadhimisho ya siku ya Malaria Afrika ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 Aprili, kwa Zanzibar mwaka huu yataadhimishwa tarehe 22 Aprili katika Ukumbi wa Idriss Abdulwakil Kikwajuni.


Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la usafi, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk. Fadhil Muhd Abdalla alisema kuondosha uchafu na mazalia ya mbu ni muhimu katika kumalliza kabisa maradhi hayo ifikapo mwaka 2023.
Dk. Fadhil alisema kiwango cha Malaria Zanzibar sio kibaya lakini baadhi ya maeneo hasa ya Mkoa Mjini Magharibi yanaonekana kuongezeka kwa maradhi hayo.

Hata hivyo alieleza kuwa agonjwa wengi wanaogundulika kuugua malaria wengi ni waliotoka nje ya Zanzibar ama Wazanzibari waliosafirki nje ya Zanzibar kwa shughuli zao mbali mbali.

Aliwashauri wananchi wanapoona dalili za kuugua malaria kwenda vituo vya afya kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu ili kuwanusuru wananchi wengine kuambukizwa maradhi hayo.

Aidha aliwataka wananchi kuendelea kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa, kuendeleza usafi katika maeneo yao na kuondosha mazalia ya mbu hasa katika kipindi hichi cha mvua za masika ili kujiepusha na Malaria na maradhi mengine.



Kaimu Meneja wa Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Dk. Faiza Bwanakheri Abass alisema wameamua kuunda Kamati za Shehia za kuimarisha usafi na kuondoa Malaria ikiwa ni moja ya njia ya kuihamasisha jamii kushiriki katika mapambano hayo.
Afisa uhamasishaji Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Dk. Mwinyi aliwataka wanchi wanaogundulika kuugua malaria waweke anuani zao kamili kwani wanakuwa wanafanya ufuatiliaji kwa kila mgonjwa ili kujua maendeleo yake na afya za majirani zake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad