Mtibwa,Kagera hali tete ligi kuu Muungwana Blog · Muungwana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Klabu ndugu za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zimepoteza mechi zao za leo za ligi kuu Tanzania bara na hivyo kuleta mashaka ya kubakia kwa msimu ujao.
Mtibwa ilipoteza 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mechi iliyochezwa mapema saa 8 :00 mchana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, magoli ya wageni yalifungwa na Abdulaziz Makame naTariq Seif katika kipindi cha kwanza na lile la wenyeji lilifungwa na Kelvin Sabato katika kipindi cha pili.

Kagera Sugar wao walipoteza 2-1 dhidi ya Biashara Mara kwenye mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa sana uliyochagizwa na kocha Francis Baraza kuzifundisha timu zote mbili hizi kwa awamu tofauti kulifanya morali ya mechi kuwa juu sana

Kupoteza kwa Mtibwa na Kagera kunaziweka timu hizi zenye nasaba katika wakati mgumu wa kushuka daraja, kwa sasa Mtibwa ipo katika nafasi ya 14 kati ya timu 18 na Kagera Sugar ipo katika nafasi ya 16 kati ya timu 18 na kwa mujibu wa kanuni timu ,4 zinashuka moja kwa moja msimu huu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad