Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Muhimbili Wamjibu Kigwangalla ‘Hatuondoi Nyungu’

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema haitaondoa huduma ya kujifukiza Hospitalini hapo kama ilivyoshauriwa na Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla, kwakuwa iko kwenye utekelezaji sahihi wa majukumu yake ya kitafiti kama wanavyofanya Wanasayansi wengine kote Duniani.

 

 

 

Taarifa iliyotolewa leo na Aminiel Aligaesha, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH imesema;

“Kuna ujumbe wa sauti ya Mbunge Kigwangalla unaosambaa kwenye mitandaoni ambao pamoja na mambo mengine anataka huduma ya kujifukiza iliyoanzishwa Muhimbili kuvunjwa kwa kuwa inaleta picha mbaya, Covid 19 ni ugonjwa mpya ambao hadi sasa Duniani hakuna mwenye majibu sahihi, majibu sahihi yanatokana na tafiti zinazofanywa sehemu mbalimbali.

 

 

 

“Kwa muda kumekuwa na taarifa kuwa tiba asilia ikiwemo kujifukiza kunasaidia katika tiba ya Covid 19, tafiti mbalimbali kutoka sehemu nyingine Duniani kama Israel na Italia zimeongelea kujifukiza (steam therapy) kama njia mojawapo ya tiba ya ugonjwa huu na mengine ya upumuaji, MNH iliona kuna umuhimu wa kuleta huduma hii ili Wananchi walio tayari waitumie na pia Wataalamu wapate nafasi ya kuifanyia utafiti kwa njia za kisayansi na kutoa majibu sahihi kama inafaa au haifai.

 

 

 

“Hii itatoa nafasi kwa Wataalamu wetu kuwa sehemu ya mjadala wa tiba ya Covid 19 badala ya kusubiri kila wazo au jibu kutoka kwa wenzetu, na hii pia inawakumbusha Wataalamu wetu wawe tayari kufanya utafiti na kuchangia kutoa majibu yanayohitajika badala ya kusubiri kila kitu tufanyiwe na kuletewa mezani.

 

 

 

”Mpaka sasa zaidi ya Wananchi 1,100 wakiwemo Wataalamu wa Afya (Madaktari, Wauguzi n.k) waliotumia huduma hii wametoa taarifa ya kuridhishwa na huduma hii,” imesema Hospitali Muhimbili.
 

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments