google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Naibu Waziri Gekul: Basata hakikisheni wasanii wanasajiliwa na kujua idadi yao kamili na wapi walipo | UDAKU SPECIAL

Naibu Waziri Gekul: Basata hakikisheni wasanii wanasajiliwa na kujua idadi yao kamili na wapi walipo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amelitaka Baraza la Kiswahili la Taifa kuongeza kasi ya kuratibu mpango wa kuwa na vituo vya kufundishia lugha ya Kiswahili kupitia balozi zetu mbalimbali nje ya nchi.



Pia Gekul amelitaka BAKITA kuhakikisha linafuatilia kwa karibu na kuhakikisha kuwa maelekezo ya viongozi wa Kitaifa kuhusu kubadili sheria na kanuni mbalimbali zilizo katika lugha ya kingereza kuwa katika lugha ya kiswahili yanafanyiwa kazi kwa haraka.

Aidha Mhe. Gekul ameielekeza Bodi ya Filamu Tanzania kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kukamilisha kwa wakati mfumo wa kielektroniki wa usajili wa Wasanii hapa nchini.

“Hakikisheni mnawasajili na kuwafikia wasanii wote nchini ili kujua idadi yao kamili na wapi walipo ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwamo mikopo na mafunzo ya kuwaongezea ujuzi” – Gekul

Mhe. Gekul ameyasema hayo leo tarehe 27/04/2021 alipokutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya BAKITA na Bodi ya Filamu Tanzania ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzitembelea Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad