Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Namungo Vs Nkana Leo… Mkishindwa Semeni Tuwasaidie

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
HUU ni mchezo wa kufa au kupona kwa Namungo katika kusaka pointi tatu mbele ya Nkana FC baada ya kupoteza michezo miwili kwenye Kundi D ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Kocha Mkuu, Hemed Morocco, leo Jumapili atakuwa na jeshi lake la Namungo kukabiliana na Wazambia hao, huku akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Mkapa kwa mabao 2-0 dhidi ya Pyramids.


Mechi hiyo ambayo itapigwa Uwanja wa Mkapa, mashabiki 10,000 wameruhusiwa kuingia.


Mashabiki hao baada ya kuona wawakilishi wao kuanza vibaya, wamewaambia ‘Mkishindwa semeni tuwasaidie.’Kwenye Kundi D, Namungo na Nkana hazijavuna pointi yoyote baada ya kucheza michezo mi-wili na kupoteza.Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Namungo, Godfroid Okoko, alisema kuwa: “Tutawakosa wache-zaji wawili akiwemo Abdulhalim Humud na Carlos Protas, lakini tofauti na hao hakuna majeruhi, wote wapo fi ti na wana morali ya kupambana ili kupata pointi tatu kwenye mchezo huo muhimu.


”Kwa upande wa Nahodha wa Namungo, Reliants Lusajo, alisema: “Utakuwa ni mchezo wa fainali kwa upande wetu, tutahakikisha tuna-pambana ili kupata pointi tatu.


”Naye Kocha Mkuu wa Nkana, Kelvin Kaindu, alisema: “Tumemaliza maandalizi licha ya kukosa kufanya maz-oezi kwenye uwanja wa mchezo, lakini tupo tayari kucheza kesho (leo).


“Tunajua kitu gani tunakihi-taji kwenye mchezo huo, lakini kila timu inahitaji kupambana kwani tupo kwenye nafasi za mwisho kwenye kundi letu.


”Richard Ocran ambaye ni Nahodha wa Nkana, alisema: “Tupo tayari kucheza na kuipambania timu kwani maandalizi yote yapo sawa.”Timu zote zikiwa zimecheza michezo miwili, Namungo ni imara kwenye upande wa ulinzi ambapo imeruhusu mabao matatu, huku Nkana ikiruhusu matano. Zote hazijafunga bao.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments