Ndugai: Uwaziri ni cheo cha muda , Bungeni Ni Nyumbani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametoa somo kwa mawaziri na manaibu akiwataka kutekeleza vyema majukumu yao na kutosahau kuwa ni wabunge na uwaziri ni vyeo vya muda.

Ndugai ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 mara baada ya kuwaapisha wabunge watatu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambao ni mabalozi, Bashiru Ally, Liberata Mulamula na Mbarouk Nassor Mbarouk.

Amesema ni vema Mawaziri na Naibu Mawaziri kufahamu bungeni ni nyumbani, na huko kwingine wanapokwenda ni matembezini, na endapo kitatokea chochote wanarudi nyumbani (Bungeni).

Spika Ndugai amewashauri Wabunge wanapoteuliwa kushika nyadhifa za Uwaziri ama Naibu Mawaziri kutolidharau Bunge na badala yake waendelee kushirikiana na Wabunge wenzao katika kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.
“Nyinyi ni wabunge kama sisi hilo ndiyo la msingi yaani hapa bungeni ndiyo nyumbani, huko mmekwenda matembezi tu likitokea jambo la kutokea mnarudi hapa.  Kwa hiyo tusisahauliane sana jamani mtapata ushauri mwingi huko Serikalini lakini msisahau kuwa ushauri wa wabunge ni muhimu sana kwa sababu ni ushauri wa wananchi,” amesema Spika Ndugai.

Amewataka Wabunge hao walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuapishwa hii leo, kwenda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa Liberata Mulamula ambaye pia ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbarouk Nassoro Mbarouk aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.Mbunge mwingine aliyeapishwa hii leo ni Dkt. Bashiru Ally.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad