Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Niyonzima Afafanua Ishu ya Kustaafu Soka

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

KIUNGO wa Yanga na Timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima, amesema hajafikia uamuzi wa kustaafu kuichezea Rwanda kama ambavyo vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikiripoti.

 

Niyonzima amekuwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda kwa muda wa miaka kumi, huku akicheza zaidi ya michezo 100.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Niyonzima alisema: “Watu wengi hawakunielewa vizuri nini nilitaka kuwasilisha katika maelezo yangu kuhusu kuichezea timu ya Taifa niliyoyatoa hivi karibuni.

 

“Nilichotaka kumaanisha ni kwamba, iwapo Rwanda ingefanikiwa kufuzu kucheza michuano ya AFCON ya mwakani basi baada ya michuano hiyo ningestaafu.

 

“Lakini kwa bahati mbaya hatujafanikiwa kufuzu, basi siwezi kufanya hivyo kwani bado kuna malengo yangu binafsi ambayo nataka niyatimize nikiwa na kikosi cha timu ya Taifa.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA JOEL THOMAS

Post a Comment

0 Comments