Okwi Awatembelea Simba Kambini Kuwamaliza Waarabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KIKOSI cha Simba kinachojiandaa na mchezo wao wa mwisho katika hatua ya makundi leo jijini Cairo kwenye mashindando ya Ligi ya Mabingwa Afrika mapema leo wamepata ugeni kwa kutenbelewa na mshambuliaji wao wa zamani Emmanuel Okwi.

 

“Emmanuel Okwi leo ametutembelea hapa kambini jijini Cairo, Misri na kupata chakula cha mchana na wachezaji pamoja na kututakia mchezo mwema wa leo usiku ambao tutawakabili Al Ahly”, Twitter ya Simba imeandika


Okwi anaecheza soka nchini Misri katika timu ya Al Ittihad Alexandria Club aliyojiunga nayo 2019 akitokea Msimbazi, timu yake hadi sasa inashikilia nafasi ya pili katika msimamo nyuma ya Zamalek katika michezo 17 iliyoshiriki huku akiwa amefunga magoli 2.

 

Simba ambao ndio vinara wa kundi A wakiongoza kwa jumla ya alama 13, katika mashindano ya Caf ikifuatiwa na wapinzani wao Al Ahly.Wekundu hao wa msimbazi wanajiandaa na mchezo wao wa mwisho katika kundi hilo dhidi ya wababe wa Misri Al Ahly, mchezo huo unapigwa majira ya 3.00-Usiku kwa Misri na 4.00 kwa majira ya Tanzania.

Simba ikienda katika mchezo huo ikiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo katika kundi hilo ikishinda michezo minne na kutoa sare moja dhidi ya Al-Merrikh kule Khartoum Sudan.Simba hadi sasa ikitajwa kama timu namba mbili kwa ubora katika mashindano hayo ikiwa na nyota kama Clotus Chama na Luís Miquissone, huku Mamelod Sundowns ikiongoza kwa ubora.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad