Penzi la Jennifer Lopez na Rodriguez Laota Mbawa
BAADA ya kuwepo kwa uvumi wa wiki kadhaa kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi wa mwanamuziki nyota na mchezaji sinema, Jennifer Lopez  (J lo) na mchumba wake Alex Rodriguez, hatimaye wawili hao wamethibitisha kuvunjika kwa uchumba wao huo na kusema, wangependelea kubaki marafiki zaidi.

 

Katika taarifa yao ya pamoja wawili hao wamesema kupitia tovuti ya Dail mail ya Uingereza,: ‘Tumetambua kuwa ni vema tukabaki marafiki na kuendelea kushirikiana katika kazi za pamoja na kusaidia kwa kila mmoja wetu kwenye biashara tulizoshirikiana pamoja na miradi.

 

‘Tunapenda kutakiana kila la kheri kwa kila mmoja wetu na watoto. Nje ya kuwaheshimu wao, maoni yetu yatakuwa ni kusema asante kwa kila aliyetutumia maneno ya faraja na kutuunga mkono’.

 

Wawili hao walianzisha mahusiano yao miaka minne iliyopita na kuchumbiana miaka miwili baadaye kabla ya kufikia tamati na kupokelewa na maoni tofauti kutoka kwa wafuasi wao.đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad