Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Prince Dube Atabiriwa Makubwa Azam FC
KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, amefunguka kuwa straika wa timu hiyo, Prince Dube ana nafasi kubwa ya kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na kasi yake ya ufungaji.

 

 

Dube raia wa Zimbabwe, alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 2-0 walioupata juzi Ijumaa dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliopigwa Dimba la Azam Complex, Dar.

 

 

Mabao hayo yamemfanya Dube kufi kisha kumi akiwa kinara akiwazidi washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na John Bocco ambao awali walikuwa wakiongoza kila mmoja akifunga mabao tisa.Akizungumza na Spoti Xtra, Bahati raia wa Burundi, amesema:

 

“Dube ni mchezaji mzuri ninafurahishwa na kiwango chake, tangu apone majeraha yake amekuwa kwenye kiwango bora, kwa uwezo ambao ameendelea kuuonesha kwa kiasi kikubwa ana nafasi ya kutwaa Tuzo ya Ufungaji Bora.”

HUSSEIN MSOLEKA, Dar

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments