Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Prof Jay afunguka kuhusu deni kubwa analodaiwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMkongwe wa muziki wa HipHop Bongo Proffesor Jay, amesema ana deni kubwa sana analodaiwa kutoka kwa mashabiki zake ambao walim-miss kipindi yupo Bungeni anatumikia wananchi wa Jimbo la Mikumi.


Katika kulipa deni hilo msanii huyo ametangaza kuja na Album yake mpya itakayotoka mwaka huu ambayo itakata kiu ya mashabiki wake ambao wamem-miss kwa kipindi kirefu alichokaa bila kutoa wimbo.


"Nilikuwa nina deni kubwa kwa mashabiki, nataka niwape furaha waliyo-miss kwa muda mrefu, nitakuja na Album mwaka huu, mimi ni Shule pia Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Kitaa na nitawaletea Album ambayo itakuwa kama kitabu na nyimbo zake zitakuwa kama Chapter"


"Napenda kuimba wimbo ambao unagusa maisha ya jamii zaidi kuliko mimi, kati ya nyimbo zangu zote chemsa biongo ningeipa tuzo za Grammy" ameongeza Prof Jay


Kwa sasa Prof Jay anatamba na wimbo wake mpya wa 'utaniambia nini' ambao unafanya vizuri kwenye vituo vingi vya Radio na TV pamoja na Digital Platform.

Post a Comment

0 Comments