Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Profesa Kabudi Aombwa Akalale Magereza "Ukimpeleka Kule Mtu Hana Hatia Huta Baki Salama"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Mbunge wa Mlimba kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Godwin Kunambi, amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, endapo itampendeza asiwe anaenda magereza kutembelea tu na kuondoka bali awe analala ili kuona hali na mazingira yalivyo huko.


Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 28, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akitoa mchango wake katika mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo iliyosomwa Bungeni hii leo.


"Mh. Waziri nishauri kitu ikikupendeza usiende tu kutembelea magereza nenda kalale, amka asubuhi utaona habari ya magereza, ndugu zangu kama kuna jambo gumu ni magereza, ukimpeleka mwanadamu kule hana hatia kilio na masikitiko yake hutabaki salama, naomba tuwe na umakini mkubwa katika suala zima la utoaji wa haki", amesema Kunambi

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments