Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Putin ndie mwanaume mwenye mvuto Urusi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Rais wa Urusi Vladmir Putin amepigiwa kura kwa mara nyingine tena mwaka huu kuwa ndie Mwanaume mwenye mvuto zaidi nchini Urusi, hii sio mara ya kwanza kwa Putin kushinda huku picha inayomuonesha akiwa bila shati ikionekana kutajwa kuwa ni bora na wapiga kura wengi.


Katika kura 2,000 zilizopigwa Putin mwenye umri wa miaka 68 amezidi kwa kura na ametangazwa Mshindi akiwashinda Waigizaji, Waimbaji, Wanamichezo na Watu wengine alioshindanishwa nao.


Shindano limeendeshwa na Mtandao wa Super Job na wamehojiwa Wanawake 1000 na Wanaume 1000 kutoka Miji 300 ya Urusi March 22 hadi March 31, Wanaume waliompigia kura Putin ni 18% na Wanawake 17% na kumfanya awe Mshindi ukilinganisha na kura walizopata wengine.


Baadhi ya Watu wanasema huenda Warusi wanampa ushindi Putin kwakuwa ni Rais na huenda wengine wana hofu ya kuchukuliwa hatua kama wasipompa kura yeye.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments