Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Safari ya Lupita Nyong’o Serengeti Yazua Gumzo Kenya

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
                                                   Lupita Nyong’o akifurahia mandhari kwenye mbuga ya Serengeti

MUIGIZAJI maarafu kutoka Hollywood, Marekani Lupita Nyong’o (38), amezua gumzo nchini Kenya baada ya kuitembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti hivi Aprili 7, 2021, hali ilizua sintofahamu miongoni mwa wakenya wakihoji safari hiyo wakati kwao pia kuna mbuga za wanyama.

 

 

Akiwa Serengeti alitumia ukurusa wake kwenye mtandao wa Instagram kuweka picha mbalimbali akionekana madhari matata kwenye mbuga hiyo.

 

 

Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walioneshwa kukasirishwa na kitendo cha Lupita kutembelea mbuga ya Serengeti wakisema ni kukosa uzalendo kwenda kutangaza utalii wa nchi nyingine.

 Baada ya kutoka Serengeti aliungana na baba yake Peter Anyang’ Nyong’o ambaye ni Gavana wa Kisumu, kwenye mkutano wa kampeni.

 

 

Lupita ambaye ni mzaliwa Mexico mwenye Asili ya Kenya, ameibuka kuwa mmoja wa waigiza maarufu kwenye kiwanda cha filamu nchini Marekani.

 

 

Filamu zilizompa umaarufu zaidi Lupita ni pamoja na 12 Years a Slave iliyotoka mwaka 2013, na Black Panther iliyotoka mwaka 2016.

Post a Comment

0 Comments