Saido Apewa Jukumu Zito Yanga


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’, amepewa jukumu zito na kaimu kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi kwa kuhakikisha anapambana na wachezaji wenzake kuisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa msimu huu.

Mwambusi leo Jumamosi ataiongoza Yanga katika mchezo wake wa kwanza akiwa kaimu kocha mkuu dhidi ya KMC katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa huku ukiwa ni mchezo wake wa kwanza baada kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Cedric Kaze.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumamosi limezipata kutoka ndani ya timu hiyo, kiungo huyo ni mmoja kati ya wachezaji waliopewa majukumu makubwa na kocha huyo kwa kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa msimu licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa Simba.

 

“Mikakati imekuwa mingi sana kwa kuwa timu inataka kupata ubingwa na ndiyo limekuwa lengo kubwa kwa sasa maana wapo wachezaji waliotakiwa wabadilike na wapo waliopewa majukumu kutokana na uzoefu wao.

 

“Sasa mtu Ntibazonkiza kocha ametaka kwanza kujitoa na kuendelea kuwa kiongozi ndani na nje ya uwanja kutokana na uzoefu wake lakini kuhakikisha Yanga inapata matokeo zaidi katika kila mchezo ambao itacheza,” alisema mtoa taarifa.

 

Saido aliyejiunga na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu, mpaka sasa ameifungia timu hiyo mabao matatu katika michezo mitatu aliyocheza kwenye ligi kuu.đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad