Saido Apewa Program Maalum Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, ameanza mazoezi katika timu hiyo kwa program maalum kabla ya kuungana na wenzake katika mazoezi ya pamoja.

Hiyo ikiwa ni siku moja tangu kiungo huyo atue nchini akitokea kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Burundi ikitoka kucheza michezo ya kuwania kufuzu AFCON.

 

Staa huyo amekosekana ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kuuguza maumivu ya nyonga.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, meneja wa timu hiyo, Hafi dh Saleh, alisema kiungo huyo alijiunga na kambi hiyo Jumamosi iliyopita akitokea kwao Burundi.

 

Saleh alisema mara baada ya Saido kutua, haraka alianza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya leo Jumanne kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

 

Aliongeza kuwa timu hiyo inaendelea vizuri katika kuelekea mchezo huo dhidi ya KMC, morali ya wachezaji ni kubwa katika kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye ligi.

 

“Timu inaendelea vizuri na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya KMC, Saido tayari yupo kambini na ameanza mazoezi kwa program maa-lum chini ya Kocha Mwambusi (Juma).

 

“Kurejea kwa Saido kutaimarisha kikosi chetu kuhak-ikisha timu in-apata ushindi katika michezo ijayo ya ligi ili tuendelee kukaa kileleni,” alisema Saleh.

STORI: WILBERT MOLANDI

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad