Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Siku 21 Maombolezo Kifo cha Magufuli Kumalizika Leo

LEO Jumanne Aprili 6, 2021 ndio siku ya mwisho ya maombolezo ya siku 21 za kifo cha rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

 

Magufuli alifariki dunia katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo na kuzikwa Machi 26, 2021 wilayani Chato Mkoa wa Geita.

 

Rais Samia alitangaza siku 21 za maombolezo huku bendera zikipepea nusu mlingoti katika kipindi hicho chote huku televisheni mbalimbali nchini zikipiga nyimbo za maombolezo.

 

Kumalizika kwa siku hizo za maombolezo maana yake ni shughuli mbalimbali kurejea kama kawaida zikiwemo sherehe.

 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments