Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Simba yataja majembe yatakayorithi mikoba ya Mnigeria

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


JUNIOR Lokosa, mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba kwa ajili ya mashindano ya kimataifa amepata warithi wake kwenye Ligi ya Mabingwa ambao ni Chris Mugalu, Meddie Kagere na John Bocco.
Lokosa raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba akitokea Klabu ya Esperance ya Tunisia Januari, mwaka huu ila kwa sasa tayari ameshasepa Bongo kutokana na uwezo wake kuwa chini ya matarajio ya benchi la ufundi la Simba.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, raia wa Ufaransa alisema kuwa hana mashaka kuhusu kutokuwepo kwa Lokosa kwa sababu anao wachezaji wengine katika nafasi hiyo.

“Kwa kweli nimezungumza sana kuhusu Lokosa,(Junior) ila ngoja niweke wazi kuwa kwa nafasi ambayo anacheza wapo wachezaji wenye uwezo wa kufanya vizuri, yupo Mugalu, (Chris), Kagere, (Meddie) na Bocco, (John).

“Kikubwa ambacho ninafurahi ni kwamba wachezaji wote waliopo wanafanya kile ambacho ninawaelekeza na wanakifuata kwa wakati,” alisema Gomes. 

Post a Comment

0 Comments