Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Spika Ndugai amtupia madongo Mbowe

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema jimbo la Hai limepata mbunge anayewawakilisha vyema tofauti na mbunge wa jimbo hilo aliyepita, hali inayoashiria kumtupia kijembe Freeman Mbowe ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo.


 

Ndugai amesema hayo leo Bungeni, Dodoma mara baada ya Mbunge Jimbo hilo Saasisha Mafuwe kuhoji ni lini serikali itatekeleza ahadi ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KIA) ambao ni wa muda mrefu na unasababisha wananchi kukosa maeneo ya malisho na kuishi kwa wasiwasi.


"Kwa kweli niwaambie wananchi wa Hai sasa mbunge mnae, maana kabla ya hapo walikuwa wanambunge anazurura zurura tu kila mahali, haulizi maswali bungeni, haeleweki eleweki sasa hongereni sana mbunge mnae kabisa," amesema Spika Ndugai bila kumtaja jina Mbowe.


Jimbo la Hai kabla ya kutwaliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa 2020 lilikuwa lipo chini ya mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Post a Comment

0 Comments