Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Suala la Kukamata Wasanii na Watu Binafsi Wanaoweka Kazi Zao Mtandaoni Lajadiliwa na Serikali

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri Innocent Bashungwa pamoja na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari chini ya Waziri Dr. Faustine Ndugulile jana zimetatua changamoto mbalimbali zinazotokana na sheria na tararibu za TCRA katika sekta za utangazaji na sanaa.

Kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo kilifuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, miongoni mwa mambo mengi waliyoagiza ni pamoja kufanyia marekebisho haraka suala la kuwachukulia hatua Wasanii na Watu wengine binafsi wanaotangaza tu kazi zao au biashara zao tu mitandaoni (sio maudhui ya habari) kwa madai kuwa hawajasajili TV zao za mitandaoni au Chaneli zao za YouTube TCRA, kwakuwa linadumaza sekta za ubunifu.

Post a Comment

0 Comments