Ukiacha Pombe Mezani Ukaenda Kujisaidia Umekwisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






JESHI la Polisi Mkoa wa Njombe limekamata magari matano ya wizi yaliyoibiwa katika sehemu mbalimbali hapa nchini, huku watu wawili wakikamatwa kuhusika na wizi huo.

 

 

Akizungumza Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issa amesema Kwamba wizi wa magari hayo umekuwa ukifanywa kwa mbinu tofauti ikiwa ni pamoja na kutumia vilevi maarufu kama dorome ili kufanikisha wizi huo.

 

 

“Taratibu za wizi wanaoiba siku hizi, ndugu zangu mnaotumia vinywaji endapo utakuwa unakunywa maji kama utakuwa umeenda kujisaidia baada ya muda na umeacha kinywaji chako usiendelee kukitumia tena kuna mtindo unaitwa ‘dorome’, dorome ni inachukuliwa ugolo ama valium inawekwa kwenye glass ama chupa ukinywa unalewa bila kujitambua na matokeo gari linaibiwa.”

 

 

“Kwa hiyo tunawasihi wananchi unapokuwa kwenye kilevi na unakuwa na mtu ambaye umfahamu anagalia usalama wako kwanza, sasa hivi hawa wenye magari haya waje wayatafute ama wayafutae na wayachukue magari yao” amesema Kamanda Hamisi Issa.

 

 

Pia ameelezea kuibuka kwa mtindio usio wa kawaida ambao watu wamekuwa wakiingia kwenye nyumba ya ibada na kuanza kuiba vifaa vinayotumika kwenye ibada.

 

 

Kuhusu masuala ya watu kupoteza maisha Kamanda Issa anasema tatizo la watu kujinyonga bado ni tatizo mkoani Njombe pamoja na masuala ya kishirikina nayo yamekuwa bado ni changamoto licha ya Kukabiliana Nayo Kwa Muda mrefu mapaka sasa.

 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad