Wanaswa na Polisi Wakijifanya Wana Ulemavu




Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limewakata watu watatu eneo la Himo Wilaya ya Moshi kwa madai ya kujifanya wana ulemavu na kuomba msaada katika maeneo mbalimbali.

 

 

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Jumanne Aprili 20, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale amesema walikamatwa Aprili 19, 2021.

 

 

“Wakina mama hawa wawili wanakaa mahali wanaomba na Watanzania wenzetu wanawahudumia wakijua ni walemavu wanahitaji msaada, lakini ni watu wenye viungo vyote na wanaweza kutembea na kujipatia riziki kwa njia halali, lakini yupo pia kijana mmoja anayewapitisha maeneo mbalimbali,” amesema.

 

 

Kamanda Kakwale ametoa wito kwa wananchi wanaojishughulisha na biashara ya kuomba wakijifanya ni watu wenye ulemavu, kuacha mara moja.

 

 

“Nitoe wito kwa wananchi waache kumbeza Mungu na kukosoa uumbaji wake kwa kujifanya walemavu huku wakiwa na viungo vyote, watumie viungo vyao kufanya kazi halali ili kupata riziki halali, wasiwahadae watu kuwa wana mapungufu ya viungo,” amesema.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad