Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wanawake Wanaojihusisha na Biashara ya Ngono Dar Kupelekwa Chanika Kujiendeleza KiuchumiMkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema wamekuja na mkakati wa kuwakamata na kuwawezesha Wanawake wanaofanya biashara ya ngono kwa kuwaweka katika eneo moja lililopo Chanika ili waweze kufanya shughuli za kilimo na ufugaji

Biashara hiyo imeonekana kushika kasi Wilayani Ilala na ugumu wa maisha umetajwa kuwa sababu kubwa ya Wanawake hao kufanya vitendo hivyo

Amesema mkakati huo unalenga kudhibiti biashara hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya Watanzania, na Wanawake watapata fursa ya kutengeneza fedha kihalali na kujijenga kiuchumi

Kwa mujibu wa DC Mjema, wapo mbioni kukamilisha taratibu za kuandaa eneo hilo na utakapokamilika, Wanawake watakaokamatwa watafikishwa hapo moja kwa moja na kufundishwa mbinu za kujiendeleza

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments