Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wawa: Hakuna wa Kuzuia Ubingwa Simba


BEKI wa kati wa Simba, Muivory Coast, Pascal Wawa ameibuka na kuweka wazi kuwa kutokana na ubora wao kwa sasa haoni atakayeweza kuwazuia kutetea ubingwa wao msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

 

Wawa ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Wawa alisema: “Nadhani bado tupo kwenye ubora ndiyo jambo kubwa la kumshukuru Mungu kwa sababu licha ya ushindani na ugumu wa ligi lakini bado tumekuwa na uwezo wa kupata matokeo bora zaidi kwa upande wetu.

 

“Kiukweli naamini nafasi ya kutetea ubingwa wetu ipo wazi na hakuna ambaye anaweza kuzuia hilo kwa sasa kutokana na kuwa kwenye kiwango bora cha ushindani, kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa ni kushinda mechi zetu ili malengo yatimie bila ya kuangalia nani anaongoza ligi,” alisema Wawa.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments