Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amefanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Mwendokasi eneo la gerezani ambapo amemuhoji Meneja kuhusu idadi ya magari aliyonunua kuongezea kwenye yale yaliyonunuliwa na Serikali.
Serikali ilinunua magari 140 ambapo hadi sasa ni magari 100 yanayofanya kazi, hali inayowapa shida Wananchi wa Kimara ambao hulazimika kupitia dirishani kutokana na uchache wa magari
Aidha Waziri Mkuu amebaini mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi. Mtendaji Mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya msambazaji na aliyeununua