Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Yanga Wajibu Mapigo ya Simba

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

BAADA ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kuweka wazi kuwa timu hiyo ipo katika mipango ya kupata basi jipya, uongozi wa Yaanga nao umejibu mapigo kwa kubainisha kwamba, wao watashusha basi jipya na kali zaidi ya hilo la Simba.

 

Simba na Yanga zote zinamiliki magari aina ya Yutong ambayo walipewa ikiwa ni sehemu ya udhamini mwaka 2012 ambayo wameyatumia kwa zaidi ya miaka tisa.

Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema kuwa klabu hiyo ipo katika mpango wa kununua basi jipya na la kisasa ambalo litakuwa bora zaidi ya lile la Simba ambalo picha zake zimekuwa zikisambaa mitandaoni.

“Yanga tupo katika mpango wa kushusha basi jipya kali kuliko lile Tata la wenzetu (Simba), sio kwamba mpango huu ni baada ya kuona wenzetu wameanza, hapana, bali ni mpango ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu.

“Hivyo wapenzi wa Yanga wanatakiwa kutulia kwani tutashusha basi jipya na kali kwa ajili ya safari za wachezaji za hapa na pale,” alisema kiongozi huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments