Abiy: Mataifa yenye nguvu 'yanafanya kampeni dhidi ya Ethiopia'
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa hatakubali uchaguzi mkuu uliocheleweshwa kutumiwa "kwa maslahi mataifa ya nje", Shirika la Habari la Ethiopia (ENA) linalomilikiwa na serikali liliripoti.
"Uchaguzi utaamuliwa na Ethiopia na Waethiopia tu, sio kutimiza maslahi ya watu wa nje," ENA ilimnukuu Abiy akisema wakati wa uzinduzi wa eneo la viwanda katika Mkoa wa Afar.Bwana Abiy alishutumu nchi ambazo hakuzitaja jina kwa kufanya kampeni dhidi ya Ethiopia.

"Nchi zilizo na uchumi imara au vyombo vingine viko katika kampeni dhidi ya Ethiopia na lengo likiwa kuamua jinsi Waethiopia wanapaswa kuishi," Bwana Abiy alinukuliwa akisema.

Ethiopia imekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa Marekani na Jumuiya ya Ulaya juu ya madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mzozo wa kibinadamu kaskazini mwa mkoa wa Tigray.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE