Adam Juma awashangaa wasanii kupagawa na viewers wa Youtube
Kupitia Instagram yake Director huyu mkongwe wa muziki Tanzania ameandika kuwa:

Views hizi zinavuruga sana watu inafika sehemu tunatokwa na povu. Kama kuna aliyeona interview ya @majizzo kuna ukweli ndani ya maneno yake, kuna views nyingi haimanishi kua nyimbo imehit au inapendwa sana na kua na views chache haimanishi mziki wako haujapenya. Inasikitisha kweli kuona mtu ana views 2million alafu kigoma, geita, muheza huko nyimbo haijulikani. Kuna level ya msanii hizi views zinamsadia ila kwa wale chipukizi wanapotezwa vibaya sana kwa hii sura tunayoijenga kwenye tasnia. Ukweli unajulikana pale tu unaposimama kwenye stage sumbawanga alafu unaimba nyimbo yako yenye views 5.6m alafu mashabiki wanakuangalia tu. Wasanii msidhararu redio hasa hizi community radios ambazo zinawafikia watu moja kwa moja, tusiache kusambaza kazi zetu kutumia mifume ya ndani na nje mafanikio yatakuja tu. Kuna wengine hili swala la views ni biashara na inawalipa, views nyingi zinamlipa zaidi na haoni tabu kuinvest kwenye kuongeza kwa sababu soko lake linamruhusu kufanya hivyo. Wasanii itumieni hii tool kama makeup tu, kuna sehemu ukipaka utachekwa na usipopaka kuna sehemu utachekwa pia, najua wakubwa wamenielewa sana. Kuna mataifa ya africa wakiona msanii wetu anaviews kama hizo anaogopa na kumpa heshima na hupelekea kupewa show yenye malipo mazuri sasa hapo msanii mwenye kajiongeza kujibrand wanasema wenyewe. Views wala sio adui kihivyo km tunavyodhani ila ukweli ni kwamba Sanaa bora siku zote inaishi.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE