.

5/28/2021

Alikiba amtolea povu Daimond "Hela ikiwepo huwa inaonekana haiitaji matangazo"
 Kwa mara ya kwanza msanii AliKiba leo Alhamisi kwenye kipindi cha Leo Tena, CloudsFm amefunguka kuhusu jina Sadala ambapo ameeleza neno hilo ni jina tu kama majina mengine huku akikazia hakupenda kitendo cha Sadala kulalamika katika hali ile.
"Sadala ni jina tu kuna watu wanaitwa Sadala" ameeleza.

"Mimi kama Mtanzania sikujisikia vizuri sio kulia tu kulalamika katika hali ile lazima kuwepo na kuandikwa katika vitu kama hivyo kwenye Facebook, haijakaa vizuri" - aliongeza.

AliKiba pia ameeleza endapo hela ukiwa nayo haitaki matangazo kuwaaminisha watu una hela.

"Hela ikiwepo huwa inaonekana haiitaji matangazo na ukitangaza watu hawawezi kuamini ukikaa kimya utaonekana na watu wataamini hata debe ukilijaza mahindi ukilipiga halitoi sauti lakini likiwa tupu ukipiga linakwenda mpaka kule. Halafu Sadala wako wengi" - @officialalikiba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger