Arsenal yaichapa Chelsea
Wakati ubao wa Stamford Bridge ukisoma Chelsea 0-1 Arsenal alikuwa ni Emile Smith Rowe alipachika bao hilo la ushindi na kuipa pointi tatu timu yake.

Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Chelsea walionekana wakihitaji zaidi matokeo kwa kufanya majaribio mengi ila bahati haikuwa yao.

Chini ya Kocha Mkuu, Thomas Tuchel ilipiga jumla ya mashuti 19 na yaliyolenga lango yalikuwa matano huku wapinzani wao Arsenal chini ya Mikel Arteta walipiga jumla ya mashuti matano na mawili yalilenga lango huku moja likileta bao.

Kwa upande wa pasi, Chelsea walipiga jumla ya pasi 765 huku wapinzani wao Arsenal wakipiga jumla ya pasi 369.

 Kusepa na pointi tatu kunawafanya Arsenal wawe na jumla ya pointi 55 nafasi ya 8 na Chelsea ipo nafasi ya 4 pointi 64 zote zimecheza mechi 36.

Bingwa ashapatikana wa Ligi Kuu England ni Manchester City na amemvua ubingwa Liverpool.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE