ASAP Rocky na Rihanna Wanapika na Kupakua

RAPA wa miondoko ya Hip Hop kutoka  Marekani ASAP Rocky ametangaza kwamba yupo katika mapenzi na mwanamuziki nyota wa miondoko ya Rnb  Rihanna.

 

Rapa huyo alimuelezea Rihanna kuwa penzi la Maisha yake katika mahojiano na GQ.

 

Uvumi kuhusu iwapo nyota hao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi ulianza mapema 2013, wakati rapa huyo alipomsaidia Rihanna katika ziara yake ya Diamond World Tour.

 

“Yeye ni sawa na labda milioni wengine, Nadhani wakati unajua, unajua tu,” alisema. “Ni Yeye tu.”

 

Wawili hao walishiriki katika Video ya ASAP Rocky ya 2013 ya fashion Killa.

 

Tangu wawili hao walipoanza mahusiano ya kimapenzi , wamekuwa wakijaribu kuwazuia waandishi wa habari kuwapiga picha pamoja, taarifa hiyo ilisema.

 

Rapa huyo alisema kwamba mpenzi wake ndiye aliyeishawishi albamu yake mpya ambayo itamshirikisha Morrissey.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE