.

5/29/2021

Askari afa maji akimkimbiza mtuhumiwa

 


Askari polisi, Isaya Kawogo amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi.


Hayo yameelezwa leo Ijumaa Mei 28, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akibainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mwisenge Manispaa ya Musoma.


 Amesema askari huyo pamoja na wenzake wakiwa doria walikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kumkimbiza.


“Yule mtuhumiwa alijitosa ziwani na askari aliamua kumfuata huko huko ziwani lakini akiwa katika harakati za kumkamata alinasa kwenye nyavu na kuzama. Mtuhumiwa alifanikiwa kuimbia,” amesema Kamanda Tibishubwamu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger