.

5/22/2021

Biden: Mataifa mawili ndiyo suluhisho pekee kwa mzozo wa Mashariki ya Kati


Rais wa Marekani Joe Biden amesema chama chake cha Democratic bado kinaunga mkono Israel na anatumai makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas yatadumu. 


Akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya White House jana akiwa na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, Biden amesema kuunda mataifa mawili ndio suluhisho pekee kutatua mzozo kati ya pande hizo mbili, na ameahidi kuhamasisha mataifa mengine katika mpango wa kusaidia kuijenga Gaza upya.Biden ameongeza kuwa ni muhimu kuzingatia usalama wa Wapalestina walioko Ukingo wa Magharibi na kuwasaidia watu wa Gaza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger